Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Muumini ni yule ambaye anapofanya kitendo chema kinamfurahisha na anatarajia thawabu zake. Na anapofanya kitendo kiovu kinamfanya vibaya na anachelea adhabu yake.”

Hichi ni kitendo kilicho na thawabu na adhabu. Haijalishi kitu sawa ikiwa ni kitendo cha ulimi au ni kitendo cha viungo. Hii ni dalili inayoonyesha kuwa matendo ni katika imani. Vilevile [ni dalili inayoonyesha kuwa] matendo yanalipwa thawabu na adhabu. Muumini anafurahi kwacho ikiwa ni kitendo chema na kinamfanya vibaya ikiwa ni kitendo kiovu. Lau ingelikuwa kweli matendo sio katika imani basi yasingelipewa hadhi hii katika Uislamu.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaaswid Kitaab-ish-Sharï´ah (2/19)
  • Imechapishwa: 26/08/2020