Somo la ´Aqiydah ni muhimu zaidi kuliko chakula, kinywaji na pumzi  

Mja anaihitajia elimu hii – yaani elimu ya somo la ´Aqiydah – juu ya haja zingine zote na dharurah yake iko juu ya dharurah zingine zote. Wanavyolihitajia ni zaidi ya wanavohitajia vyakula na kinywaji. Bali analihitaji zaidi kuliko anavohitajia pumzi. Kwa sababu mtu akikosa chakula na kinywaji na pumzi mwili unakufa. Na mauti hakuna budi yatamfika tu. Haidhuru kitu mwili ukifa midhali moyo umenyooka. Upande mwingine mtu akikosa kumtambua Mola Wake, majina na sifa Zake na elimu kuhusu Shari´ah na dini yake, basi moyo wake unakufa. Hapa ndipo kunabainika haja ya waja juu ya elimu ya msingi wa dini. Hivyo ni kwa sababu hakuna uhai wa moyo, neema, utulivu wala furaha isipokuwa kwa mja kumtambua Mola Wake, Mwumbaji Wake, Anayemwendesha na Anayemwabudu kwa majina Yake na sifa Zake. Kwa hayo atakuja kumpenda zaidi ya kila kitu na juhudi na matendo yake yatakuwa kwa yale yanayomkurubisha Kwake (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (07/01)
  • Imechapishwa: 07/06/2020