´Aqiydah hii – yaani al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – katika msingi wa dini sio maalum kwa Ahnaaf. Bali ni kwa watu wote; Ahnaaf, Maalikiyyah, Shaafi´iyyah na Hanaabilah. Kufuata madhehebu fulani ni jambo linalohusiana na matawi ya Dini kama mfano wa hukumu za swalah, zakaah, swawm na hajj. Ama kuhusu ´Aqiydah na Tawhiyd ni jambo moja na hakuna tofauti.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (19/01)
  • Imechapishwa: 07/06/2020