Swali: [Sauti haisikiki]

Jibu: Jambo la kwanza Bid´ah inapaswa ijulikane. Sio kila kinachosemwa na watu kuwa ni Bid´ah inakuwa ni Bid´ah. Watu wengi wanaojifanya kuwa ni wanachuoni na wajinga wanafanya Tabdiy´ pasina elimu. Bid´ah inapaswa itambulike. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amebainisha kidhibiti chake:

“Atakayezusha katika Amri yetu hii yasiyokuwemo atarudishiwa mwenyewe.”

“Kila kitachozushwa ni Bid´ah. Kila Bid´ah ni upotevu.”

“Atakayefanya ´amali isiyokuwa na Amri yetu atarudishiwa mwenyewe.”

Yale yanayoenda kinyume au yamezidishwa juu ya yale Aliyoweka Allaah na Mtume Wake katika Shari´ah katika mambo ya ´ibaadah ndio Bid´ah. Bid´ah ni yale ambayo hayakuweka Allaah wala Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Ama kuhusu jinsi ya kutangaman na mtu wa Bid´ah, ikithibiti kama kweli ni mtu wa Bid´ah basi anasihiwe na kuwekewa wazi kuwa hii ni Bid´ah na kwamba ni upotevu. Akikubali na kuacha himdi zote ni Zake Allaah. Akiendelea na Bid´ah hizo baada ya kubainishiwa basi inachotakiwa ni kususwa mpaka atubu kwa Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Buluugh al-Maraam (13) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/blug–1430-8-13.mp3
  • Imechapishwa: 19/04/2015