Swali: Je, inajuzu kuitwa kwa jina la ´Uqaab kwa kuzingatia ya kwamba hili ni jina miongoni mwa majina ya ndege?

Jibu: Kizuizi kiko wapi? Lililokatazwa ni kuitwa kwa jina lililo la uabudiwa wa asiyekuwa Allaah. Kama kusema ´Abdur-Rasuul, ´Abdul-Husayn n.k. Majina kama haya ndio yamekatazwa. Ama kuhusu majina mengine ambayo hayana uabudiwa wa asiyekuwa Allaah hayana neno.

Hata hivyo imependekezwa kuitwa kwa jina zuri. Imependekezwa kumchagulia mtoto wako jina zuri. Hili ni kwa njia ya mapendekezo. Ama uharamu hauwepo isipokuwa tu pale ambapo jina litakuwa na uabudiwa wa asiyekuwa Allaah. Kama mfano wa ´Abdul-´Uzza, ´Abdul-Ka´bah, ´Abdur-Rasuul, ´Abdul-Husayn n.k. Majina kama haya ni haramu na hayajuzu. Ibn Hazm (Rahimahu Allaah) amesema:

“Wamekubaliana juu ya uharamu wa kila jina lililo la uabudiwa wa asiyekuwa Allaah isipokuwa tu ´Abdul-Muttwalib.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Buluugh al-Maraam (13) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/blug–1430-8-13.mp3
  • Imechapishwa: 19/04/2015