Swali: Kuna mtu jina lake anaitwa ´Abdul-Muhsin. Je, inajuzu kumwita ´Muhsin` tu kwa kuwa nimeambiwa kuwa ni Jina miongoni mwa Majina ya Allaah na hivyo haijuzu kumwita kwa jina hilo?

Jibu: Maadamu jina lake anaitwa ´Abdul-Muhsin mwite hivo. Mwite kwa jina lake kamilifu.

Lakini tukikadiria kuwa ataitwa Muhsin hakuna neno kufanya hivo. Haina neno akaitwa Muhsin. Muhsin linatokamana na Ihsaan. Mtu pia anafanya wema na anaitwa Muhsin:

إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ

“Hakika Allaah Anapenda watendao wema.” (02:195)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Buluugh al-Maraam (13) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/blug–1430-8-13.mp3