Si lazima kwa wanaoeshi Ulaya kufanya Hijrah?

Swali: Nasikia mara nyingi ya kwamba kufanya Hijrah kutoka nchi za makafir iza Ulaya sio lazima kwa sababu ipo misikiti mingi na waislamu wako katika nafasi na kuheshimiwa kwa dini yao. Je, maneno haya yanayorudiwarudiwa ni sahihi?

Jibu: Hapana, si sahihi. Hijrah haitosimama mpaka isimame tawbah, na tawbah haitokatika mpaka lichomoze jua kutoka magharibi. Haijuzu kwa mtu kuacha kuhama ilihali ana uwezo wa kufanya hivo. Ama ikiwa hawezi basi atabakia na waislamu wenzake. Sababu nyingine inayoweza kumfanya kubakia ni kwa ajili ya kulingania kwa Allaah na kuwanufaisha waislamu. Katika hali hiyo hapana vibaya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (40)
  • Imechapishwa: 18/05/2023