Nywele zake nyeusi ni nzuri na bora zaidi

Swali: Je, inafaa kwa mwanamke kupaka nywele zake rangi nyingine isiyokuwa nyeusi kwa lengo la kujipamba?

Jibu: Nywele zake za kawaida au mvi? Ikiwa nywele zake zina rangi ya weusi wa kawaida, basi asizibadilishe. Kubakia na rangi yake ya weusi ndio kuzuri zaidi na bora kwake. Lakini ikiwa nywele zake ni mvi, basi azibadilishe kwa rangi nyingine isiyokuwa nyeusi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (40)
  • Imechapishwa: 18/05/2023