Dr Ibraahiym [ar-Ruhayliy] amesema:

”Wakati anaporaddiwa ambaye ameenda kinyume mtu anatakiwa kuzingatia kutofautiana kwa ngazi ya wale wanaoenda kinyume, nafasi ya yule aliyeenda kinyume katika dini na dunia na sababu inayotokana na kwenda kinyume huko; inatokana na ujinga, matamanio au Bid´ah, utamkaji mbaya, ulimi umemteleza, ameathiriwa na mwalimu au watu wa mji wake, tafsiri au mengineyo yanayoweza kuwa nyuma ya upindaji?

Ambaye hazingatii tofauti hizi basi ataingia katika kuchupa mipaka au uzembeaji ambao utasababisha kutonufaika na maneno yake au angalau kwa uchache yanufaishe kwa uchache.”[1]

Maneno yote haya yako kijumlajumla. Tunataraji Dr Ibraahiym atayapambanua maneno haya ya kijumlajumla, atatuletea mifano na kuyasimamishia dalili. Vinginevyo yatawakanganya wasomaji wengi. Kupitia vikwazo vyote hivi anawazuilia watu kutakiana mema kwa ajili ya Allaah, Kitabu Chake, Mtume Wake, viongozi wa waislamu na wale watu wao wa kawaida.

Ni lazima kwa mwanachuoni au mwanafunzi wakati anapowaona watu wanamuomba mwingine asiyekuwa Allaah, wanachinja na kadhalika kujua tofauti ya ngazi ya wale wanaoenda kinyume, sababu iliyowafanya wao kupinda na mengineyo? Kuna dalili yoyote ndani ya Qur-aan na Sunnah juu ya hilo? Amesema (Ta´ala):

فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا

”Mkizozana juu ya jambo, basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume mkiwa mnamuamini Allaah na siku ya Mwisho. Hivyo ni bora na matokeo mazuri kabisa.”[2]

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule miongoni mwenu atakayeona maovu basi ayazuie kwa mkono wake. Asipoweza, basi afanye hivo kwa mdomo wake. Asipoweza, basi afanye hivo kwa moyo wake na hiyo ni imani dhaifu mno.”[3]

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakutaja chochote katika vikwazo hivi vilivyotajwa na Dr Ibraahiym. Licha ya kwamba Ruduud za Salaf kwa Ahl-ul-Bid´ah na watenda maovu ni nyingi, hatuoni vikwazo hivi vigumu.

Ni kweli kwamba Radd ya mwanachuoni inatakiwa iwe imejengeka juu ya Qur-aan na Sunnah na kwa njia ya sawa. Wakati fulani mazingira yanahitajia ulaini na upole, wakati mwingine yanahitajia ukali kwa yule mwenye kufanya ujeuri na ukaidi. Yote mawili hayapingani na hekima. Kwani hekima maana yake ni kule kukiweka kila kitu mahali pake stahiki.

Si lazima kwa yule mwenye kuraddi kujua sababu iliyopelekea katika Bid´ah au maasi fulani. Ni kitu ambacho Allaah pekee ndiye anakijua. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema juu ya kisa cha Dhul-Khuwayswiyrah:

”Mimi sijaamrishwa kuichimba mioyo ya watu wala kuyafungua matumbo yao.”[4]

[1] an-Naswiyhah, uk. 31

[2] 4:59

[3] Ahmad (3/10) na Muslim (49).

[4] al-Bukhaariy (4351) na Muslim (1064).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan maa fiy Naswiyhati Ibraahiym ar-Ruhayliy min al-Khalal wal-Ikhlaal, uk. 50-52
  • Imechapishwa: 16/12/2022