Mitume na wale wanazuoni wanaofuata mfumo wao wanalingania katika haki na Tawhiyd. Wanakemea batili na shirki katika kila mahali na wakati. Hawajali ni nguvu kiasi gani walionayo watu wa batili, washirikina na watu wa batili. Qur-aan imejaa visa vya Mitume namna wanavyokabiliana na washirikina, makafiri na watu wenye kiburi.

Miongoni mwavyo ni Ibraahiym, ambaye ni rafiki wa hali ya juu wa Allaah, alivyokabiliana na Namruud na watu wake.

Miongoni mwavyo ni Muusa, ambaye amezungumzishwa moja kwa moja na Allaah, alivyokabiliana na Fir´awn na watu wake.

Miognoni mwa makabiliyano ya wanazuoni ni pamoja na Imaam Ahmad alivyokabiliana na dola ya al-Ma´muun, al-Mu´taswim na al-Waathiq. Ilikuwa ni makhaliyfah wa ´Abbaasiyyah wakiwa pamoja na mahakimu na viongozi wa Jahmiyyah na Mu´tazilah.

Miongoni mwao ni makabiliyano ya Shaykh-ul-Islaam Ibn Tamiyyah na mwanafunzi wake Ibn-ul-Qayyim, Ibn ´Abdil-Haadiy na makabiliano mengine kwa Ashaa´irah na Suufiyyah licha ya kuwa wao ndio walikuwa na dola na nchi ilikuwa mikononi mwao.

Miongoni mwao ni makabiliyano ya Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab kutokana na nguvu ya shari na batili mpaka akasimamisha dola ya Kiislamu, yenye nguvu.

Hakuna yeyote katika hao waliyotajwa ambaye alichukua ruhusa ya kuacha makabiliano wakati wa udhaifu. Bali walichukua wameamua. Waliona jambo la lazima ni kuwa waamuzi na kwamba kufanya hivo ni miongoni mwa aina kubwa kabisa za jihaad. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Jihaad aina bora kabisa ni neno la haki mbele ya mtawala mnyanyasaji.”

Hii leo Ahl-us-Sunnan wamesimama katika nchi mbalimbali kwa ajili ya kulingania kwa Allaah. Wanavumilia mazito yanayowakumba katika nchi hizi ambapo utawala na nguvu yanakuwa kwa Ahl-ul-Bid´ah na watu wa batili. Hilo haliwazuii kuendelea kulingania katika haki na kufanya subiri juu ya yale mazito yanayowakuta.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan maa fiy Naswiyhati Ibraahiym ar-Ruhayliy min al-Khalal wal-Ikhlaal, uk. 41
  • Imechapishwa: 16/12/2022