Sharti mbili baba kuchukua mali ya mwanae

Swali: Ni yepi makusudio ya Hadiyth:

“Wewe ni mali yako ni milki ya baba yako.”?

Jibu: Kutokana na udhahiri wake. Baba ana haki ya kuchukua kutoka katika mali ya mwanae kwa sababu mtoto wake ni chumo la baba yake:

“Hakika mlichokula kilicho na haki zaidi ni katika mapato yenu na hakika wana wenu ni katika mapato yenu.”

Mwanamume ana haki ya kumiliki kutoka katika mali ya mtoto wake kwa sharti mbili kwa mujibu wa wanachuoni:

1- Asimdhuru.

2- Asichukue akampa mtoto wake mwingine.

Baba ana haki ya kuchukua kile kilichozidi juu ya haja ya mtoto wake kwa sharti asimpe mtoto wake mwingine na pia kitu hicho kisimdhuru. Haifai kuchukua ikiwa kunamdhuru. Madhara ni kwa mfano baba akachukua mali yake na akamwacha mtoto wake ni mwenye kuombaomba watu. Haijuzu kwa baba kufanya hivo. Lakini akichukua kitu kilichozidi juu ya haja yake na asimpe mtoto wake mwingine itafaa kwake kufanya hivo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (15)
  • Imechapishwa: 16/08/2020