Swali:  Kwenye msikiti wa kitongoji cha Nasiym nimeona kitabu kinachotawanywa sana na kichwa chake cha khabari ni “Da´naa´ Namuut hattaa Nanaal-ash-Shahaadah”.[1] Humo mwandishi anawaponda wanachuoni na kusema kuwa tumepewa mtihani kwa wanachuoni ambao hawaiti katika Jihaad. Anawatukana na kuwaponda watawala. Watu wamepewa mtihani kwa kitabu hichi. Ni lipi la wajibu?

Jibu: Huyu anasema “wache tufe.” Mwache afe. Mtu huyu kufa kwake ni bora kuliko kubaki kwake. Tuleteeni nuskha ili tuangalie.

[1] Tuache tufe ili tupate shahada. Sulaymaan al-´Ulwaan amesema:

“Ummah umetiwa kwenye mtihani na watawala ambao wamezifuta adhabu za Kishari´ah, wamesitisha Jihaad katika njia ya Allaah na kukataza Qunuut katika swalah tano. Wanachuoni wanayatakasa mambo haya yenye kutia aibu na kutetea kushindwa kwao kuunusuru Uislamu na waislamu kwa hoja kwamba ni wajibu kuwasikiliza na kuwatii watawala katika yanayopendwa na kuchukiwa.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=oGHnF2PJJtI&feature=youtu.be
  • Imechapishwa: 16/08/2020