Anataka kujitolea figo lake kumpa nduguye

Swali: Nina ndugu yangu wa damu ambaye amepatwa na ugonjwa wa figo na maambukizi khatari figoni. Nimeweka azma ya kujitolea figo kumpa. Je, inajuzu kufanya hivo? Au nende India na kumnunulia figo ndugu yangu?

Jibu: Wanachuoni wametofautiana juu ya hilo. Miongoni mwao wako ambao wamejuzisha hilo na wengine hawakujuzisha hilo. Maoni yaliyo karibu zaidi na usawa – na Allaah ndiye mjuzi zaidi – ni kujuzu kufanya hivo muda wa kuwa madaktari wataalamu wamethibitisha kuwa hakuna khatari yoyote juu yake, kwamba akichukuliwa figo basi figo lake lingine lililobaki litamsaidia na wala jambo hilo halitomdhuru, kwamba litamsaidia huyo nduguye na kwamba litatekeleza haja ya nduguye. Kwa sababu baadhi ya mafigo hayafanyi kazi. Madaktari wataalamu wa ugonjwa huo wakithibitisha na wakati huohuo hakuna khatari basi hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4285/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%AA%D8%A8%D8%B1%D8%B9-%D8%A8%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%B9%D8%B6%D8%A7%D8%A1-%D9%84%D9%84%D8%A7%D9%86%D8%B3%D8%A7%D9%86-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B6%D8%B7%D8%B1
  • Imechapishwa: 16/08/2020