Kwa hakika ile shari ambayo Allaah anamkadiria nayo mwanadamu ni kheri. Kwa kuwa mwanadamu huyo akiwa na subira na kutaraji malipo kutoka kwa Allaah, basi hupata ujira mwingi kuliko ile shari iliyomfika. Inasemekana kuna baadhi ya wafanya ´ibaadah waliojikata kwenye kidole au mkono, wakamshukuru Allaah kwa hili na kusema utamu wa ujira wake unapatikana kwa kuwa na subira.

Uhakika wa shari haiko katika kile kitendo cha Allaah kwa dhati yake, shari inapatikana kwa kile kitendo kinachofanywa. Yale matendo yanayofanywa ndio yana kheri na shari. Lakink kitendo kwa dhati yake ni kheri. Kwa ajili hii Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ مِن شَرِّ مَا خَلَقَ

“Sema: “Najikinga na Mola wa mapambazuko.Kutokana na shari ya alivyoviumba”.” (113:01-02)

bi maana kutokana na shari katika vile alivyoumba.

Shari inakuwa katika vile vinavyofanywa na si katika dhati yake kile kitendo. Kitendo cha Allaah kwa dhati yake ni kheri. Dalili ya hili ni kwa mfano wewe uko na mgonjwa na ukaambiwaya kwamba dawa yake ni kumchoma na moto na ukawa umemchoma na moto. Moto ni wenye kutia uchungu. Ni jambo lisilokuwa na shaka yoyote. Lakini hata hivyo kitendo chako hichi sio shari. Hili ni kheri kwa mgonjwa. Kwa sababu unataraji mwisho mzuri kwa kitendo hichi. Vivyo hivyo matendo ya Allaah juu ya mambo yenye kuchukiza na mambo yanayoonekana ni shari, kwa nisba ya kitendo Chake na kufanya kupatikana kwake ni kheri. Kwa kuwa kinapelekea katika kheri nyingi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/479-480)
  • Imechapishwa: 19/06/2023