Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

عن أبي ثابت، وقيل : أبي سعيد، وقيل: أبي الوليد، سهل بن حُنَيْفٍ وَهُوَ بدريٌّ رضي الله عنه : أنَّ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (مَنْ سَأَلَ الله تَعَالَى الشَّهَادَةَ بِصِدْقٍ بَلَّغَهُ اللهُ مَنَازِلَ الشُّهَدَاءِ وَإِنْ مَاتَ عَلَى فِرَاشِهِ). رواه مسلم

57 – Abu Thaabit, na imesemekana vilevile Abu Sa´iyd, na imesemekana vilevile Sahl bin Hunayf na alishiriki katika vita vya Badr ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kumuomba Allaah (Ta´ala) kufa shahidi kwa ukweli, basi Allaah atamfikisha daraja ya mashahidi hata kama atakufa juu kitanda chake.” Ameipokea Muslim.

Mtu akimuomba Mola wake na kusema:

“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba nife shahidi katika njia ya Allaah – ingawa shahada haipatikani isipokuwa vitani – ili neno la Allaah liweze kuwa juu”

Allaah (Ta´ala) endapo atajua kuwa ni mwenye kusema kweli kabisa na nia, basi Allaah atamshusha ngazi ya mashahidi hata kama atakufa kitandani mwake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/312)
  • Imechapishwa: 03/05/2023