Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

عن أبي خالد حَكيمِ بنِ حزامٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (البَيِّعَانِ بالخِيَار مَا لَمْ يَتَفَرَّقَا، فَإنْ صَدَقا وَبيَّنَا بُوركَ لَهُمَا في بيعِهمَا، وإنْ كَذَبَا وَكَتَمَا مُحِقَتْ بركَةُ بَيعِهِما). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

59 – Abu Khaalid Hakiym bin Hizaam (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wenye kuuziana wako katika khiyari muda hawajaachana. Endapo watasema kweli na kubainisha, basi watabarikiwa katika biashara yao. Na endapo watasema uongo na kuficha, basi wataondoshewa baraka katika biashara yao.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Kwa mfano mtu atakuuzia gari hii na kukumwambia kuwa ni gari mpya, ya mwaka fulani, nzuri na mengineyo katika sifa ambazo haina, huu amesema uongo. Akiuza gari na iko na kasoro na akaficha kasoro hiyo, tunasema kuwa huyu ameficha na hakubainisha. Baraka iko kwenye ukweli na ubainifu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/322)
  • Imechapishwa: 03/05/2023