Shahaadah ndio maneno yanayopendeza zaidi kwa Allaah

Swali: Hadiyth inayosema kuwa maneno yanayopendeza zaidi kwa Allaah ni:

سبحان الله وبحمده

“Allaah ametakasika kutokana na mapungufu na himdi zote njema anastahiki Allaah.”

Hadiyth nyingine tuliyosoma punde inasema:

“Dhikr bora ni ´hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah`.”

Jibu: Shahaadah ni moja katika maneno haya manne.

Muulizaji: Hapana, Hadiyth ya Abu Dardaa´ inasema ni:

سبحان الله وبحمده

“Allaah ametakasika kutokana na mapungufu na himdi zote njema anastahiki Allaah.”

Ibn Baaz: Hili linatakiwa kuangaliwa vyema. Pengine imefutwa. Inawezekana vilevile ikawa na  maana kwamba ni miongoni mwa matendo yanayopendeza zaidi kwa Allaah. Kwa sababu Hadiyth inayosema kuwa shahaadah ndio maneno yanayopendeza zaidi kwa Allaah inatamka wazi kuwa ndio maneno bora zaidi. Aidha kuna Hadiyth nyingine Swahiyh inayosema:

“Imani ni tanzu sabini na kitu. Ilio juu kabisa ni kusema “nashuhudia ya kwamba hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah… ” na ilio chini ni kuondoa chenye kudhuru njiani.”[1]

Hii inatamka wazi. Baadhi ya mambo yanafasiriwa kuwa ni miongoni mwa mambo yanayopendeza zaidi kwa Allaah.

[1] al-Bukhaariy (9) na Muslim (35).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23081/ما-الاصح-في-احب-الكلام-الى-الله
  • Imechapishwa: 27/10/2023