Hii ni dalili ya kufaa kwa mwenye janaba kusoma Qur-aan?

Swali: Hadiyth ya ´Aaishah inayosema kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akimtaja Allaah katika hali zake zote wanaijengea hoja wale wanaosema kuwa inafaa kwa mwenye janaba kusoma Qur-aan.

Jibu: Sio dalili. Hii ni Dhikr yenye kujitegemea. Tofauti katika suala hili inatambulika. Hata hivyo hiyo sio dalili. Hadiyth ya ´Aliy inatamka wazi.

Swali: Umetaja kwamba alikuwa akimtaja Allaah katika hali zake zote. Kwa hivyo zinabaguliwa hali kama vile…

Jibu: Katika kila hali inayotambulika. Kwa mfano alikuwa anavua pete yake pindi anapoingia chooni. Kwa hiyo ni jambo lenye haki zaidi kwa yeye kujizuilia na jambo hilo pindi anapokidhi haja. Isipokuwa ndani ya moyo wake, kwa sababu hapana vibaya kumtaja Allaah ndani ya moyo wako.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23082/حكم-قراءة-الجنب-القران
  • Imechapishwa: 27/10/2023