Salamu kabla ya shikamo na khabari yako

Swali: Baadhi ya watu wanapokutana asubuhi huambiana “Khabari za asubuhi”.

Jibu: Hapana. Bora ni kusema:

السلام عليكم

“Amani ya Allaah iwe juu yenu.”

Kisha baada ya kutoa salamu ndio anaweza kusema ´khabari za asubuhi` au ´vipi hali yako?`. Anatakiwa kuanza kutoa salamu. Hii ndio Sunnah. Msalimiwaji atajibu kwa kusema:

وعليكم السلام

“Nawe amani ya Allaah iwe juu yako.”

Kisha akipenda atamwambia ´vipi hali yako?`, ´vipi hali ya watoto wako?`. Hapana vibaya kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23083/حكم-قول-صباح-الخير-للتحية
  • Imechapishwa: 27/10/2023