Salama zaidi muumini asisome Qur-aan ikiwa hana twahara

Swali: Ibn Hazm amejengea hoja kitendo cha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutuma barua kwamba inafaa kwa asiyekuwa na twahara kugusa msahafu.

Jibu: Hizi ni Aayah alizoziandika kwenye barua. Haikukatazwa kuandika Aayah katika barua. Hata hivyo Hadiyth imezungumziwa na wanazuoni. Ni miongoni mwa mapokezi ya ´Abdullaah bin Salamah. Baadhi yao wamesema kuwa alichanganyikiwa na kwamba hayategemewi mapokezi yake. Wengine wakaona kuwa mapokezi yake ni mazuri. Ninachotaka kusema ni kwamba haya ni mambo ambayo wanazuoni wamekinzana juu yake. Tahadhari zaidi kwa muumini ni yeye asisome [Qur-aan] pindi anapokuwa na janaba.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23084/حكم-مس-المصحف-بغير-طهارة
  • Imechapishwa: 27/10/2023