61. Ni misafara ipi ya kijeshi ilifanyika mwaka wa 8?

Swali 61: Ni misafara ipi ya kijeshi ilifanyika mwaka huo?

Jibu: Msafara wa kijeshi wa Shujaa´ bin Wahb kwenda Hawaazin. Katika mwaka huohuo Kab bin ´Umayr akatumwa kwenda Qudhwa´ah ambapo yeye na wale waliokuwa pamoja naye wakauliwa hali ya kuwa ni mashahidi.

Imesemekana vilevile kwamba ´Amr bin al-‘Aasw alitumwa kwenda Dhaat-us-Salaasil na baada ya hapo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akamsaidia kwa Abu Bakr na ´Umar pamoja na Abu ´Ubaydah kuwa kiongozi wao. Walipofika uongozi ulikwenda kwa ´Amr bin al-‘Aasw. Katika msafara huo wa kijeshi alifanya Tayammum baada ya janaba kutokana na ukali wa baridi, kisha akawaswalisha. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akamkubalia juu ya jambo hilo.

Abu ´Ubaydah alitumwa kwenye msafara wa kijeshi hadi Siyf-ul-Bahr. Wakati wa tukio hilohilo walipata nyangumi wa manii aliyekwama. Haya yote yalitokea kabla ya Ufunguzi.

Khaalid bin al-Waliyd alitumwa kwa Banuu Judhaymah. Badala ya kusema kwamba wamesilimu ikatokea wakasema kuwa wameritadi ambapo matokeo yake wakauliwa na kukamatwa mateka. Kwa hiyo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alimtuma ´Aliy bin Abiy Twaalib kuwafanyia marekebisho ya waliouawa na kuwarudishia mali zao. Baada ya hapo akamtuma (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwenda kuvunja al-´Uzzaa. Matukio yote mawili yalitokea ndani ya muda wa Ufunguzi na Hawaazin.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 125-126
  • Imechapishwa: 27/10/2023