Du´aa ya jimaa inasomwa kimyakimya au kwa sauti?

Swali: Du´aa inayosema:

بسم الله اللهم جنبنا الشيطان وجنب الشيطان ما رزقتنا

“Naanza kwa jina la Allaah! Ee nilinde na shaytwaan na Kilinde na shaytwaan kile utachoturuzuku.”

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusiana na hili:

“Endapo Allaah amewaandikia kupata mtoto basi kamwe shaytwana hatomdhuru.”[1]

Aiseme mume baina yake yeye na nafsi yake?

Jibu: Ndio, mke asikie. Wote waseme:

بسم الله اللهم جنبنا الشيطان وجنب الشيطان ما رزقتنا

“Naanza kwa jina la Allaah! Ee nilinde na shaytwaan na Kilinde na shaytwaan kile utachoturuzuku.”

Mwanamke pia anatakiwa kusema hivo.

Swali: Je, aisome atapotaka kumwaga manii nje ya tupu ya mke?

Jibu: Aisome hata kama kumwaga manii nje ya tupu ya mke. Anaweza kutanguliwa na matamanio na asifikie lengo lake.

Swali: Lakini aisome kimyakimya?

Jibu: Aitamke.

[1] Ameipokea al-Bukhaariy katika “as-Swahiyh” yake (09/187) na waandishi wengine wa “as-Sunan” isipokuwa an-Nasaa´iy, katika “al-´Asharah” (01/79), ´Abdur-Razzaaq (06/193), at-Twabaraaniy (02/151/3) kupitia kwa Anas. Vilevile imepokelewa katika “al-Irwaa´-ul-Ghaliyl” (2012) kwa ukamilifu zaidi kuliko hapa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23086/هل-الذكر-عند-الجماع-يقال-سرا
  • Imechapishwa: 28/10/2023