Swali: Vipi kuhusu mwenye kusema kuwa kisomo chake na matamshi yake ya kisomo cha Qur-aan yameumbwa?
Jibu: Anatakiwa kusema wazi sauti yake anayosoma ndio imeumbwa. Lakini Qur-aan haikuumbwa. Akisema matamshi yake kunaleta sintofahamu. Mtu anaweza kufikiri kuwa anakusudia kile kinachotamkwa. Aseme wazi kwamba sauti yake ndio imeumbwa. Kuhusu Qur-aan ni maneno ya Allaah na hayakuumbwa.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat ´alaal-Fatwaa al-Hamawiyyah al-Kubraa, uk. 156
- Imechapishwa: 16/02/2023