Swali: Kuna mambo matano ambayo hakuna ayajuaye isipokuwa Allaah. Nini mtu aseme kuhusu kujua kwao jinsia ya kipomoko ni mme au mke?
Jibu: Inakuwa baada ya kuumbwa na baada ya Allaah kumuidhinisha Malaika aumbwe mume au mke. Baada ya Malaika kujua wanaweza kujua wengine pia. Lakini kabla ya hapo anayejua ni Allaah pekee. Baada ya mtoto kuumbwa wanaweza kujua baadhi ya mambo kwa kutumia mashine. Lakini hawawezi kufanya hivo kabla ya hapo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat ´alaal-Fatwaa al-Hamawiyyah al-Kubraa, uk. 148
- Imechapishwa: 16/02/2023