Swali: Baadhi ya wakaguzi waliokuja nyuma wamekusanya njia za Hadiyth zinazosema kuwa Allaah hushuka usiku wa nusu Sha´baan na wakasema kuwa ni Swahiyh.
Ibn Baaz: Ni Shaykh gani?
Muulizaji: Shaykh Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy.
Jibu: Mtu arejelee. Kutokana na ninavojua sio Swahiyh. Nilifuatilia hilo zamani na nikaona si Swahiyh. Anaweza kukosea katika baadhi ya mambo na baadhi ya Hadiyth.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat ´alaal-Fatwaa al-Hamawiyyah al-Kubraa, uk. 144
- Imechapishwa: 16/02/2023