Sehemu kidogo ya uchi kuonekana wakati wa kuswali

Swali: Kuna mtu anaswali na suruwali na imeraruka sehemu ya uchi uwazi kidogo na ameiswalia swalah nyingi. Je, airudie swalah yake?

Ibn Baaz: Hakuna kitu kingine alichovaa?

Muulizaji: Hakuna kitu kingine.

Ibn Baaz: Hajui jambo hilo?

Muulizaji: Alifikiri inafaa kwa sababu ni sehemu kidogo sana.

Ibn Baaz: Azinduliwe huko mbele. Azinduliwe. Pengine Allaah akamsamehe juu ya yaliyopita. Lakini anatakiwa kujikagua huko mbele ili ahakikishe amejifunika mwili mzima.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22746/حكم-صلاة-من-في-ملابسه-شق-يسير
  • Imechapishwa: 17/08/2023