Swali: Ni ipi hukumu ya anayepuuza swalah?

Jibu: Ni miongoni mwa sifa za wanafiki. Hukumu yake ni haramu. Ni miongoni mwa sifa za unafiki:

إِنَّ الْمُنَافِقِينَ يُخَادِعُونَ اللَّـهَ وَهُوَ خَادِعُهُمْ وَإِذَا قَامُوا إِلَى الصَّلَاةِ قَامُوا كُسَالَىٰ يُرَاءُونَ النَّاسَ وَلَا يَذْكُرُونَ اللَّـهَ إِلَّا قَلِيلًا

“Hakika wanafiki wanafikiri wanamhadaa Allaah na hali Yeye ndiye Mwenye kuwahadaa na wanaposimama kuswali basi husimama kwa uvivu, wakijionyesha kwa watu na wala hawamtaji Allaah isipokuwa kidogo tu.” (04:142)

Hii ni moja katika sifa za wanafiki. Ni lazima kwa muumini awe mchangamfu katika swalah, mwenye kuipupia na mwenye kuikimbilia ili asijifananishe na maadui wa Allaah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22753/ما-حكم-التهاون-بالصلاة
  • Imechapishwa: 17/08/2023