Swali: Je, tumthibitishie Allaah ulimi kwa kusema ya kwamba Qur-aan ni maneno ya Allaah ambayo ameitamka kwenye ulimi Wake?

Jibu: Hapana. Hatumthibitishii Allaah chochote isipokuwa kile alichojithibitishia yeye Mwenyewe. Hakuna dalili ya kuwa Allaah ana ulimi. Hili linapatikana kwenye tafsiyr ya Sayyid Qutwub ambapo anasema kuwa Qur-aan imetoka kwenye ulimi wa Allaah. Hili ni kosa, ni kosa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (10) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/msrf–02041434.mp3
  • Imechapishwa: 27/06/2015