Kwanini asikufurishwe al-Ma´muun aliyeita katika shirki kubwa?

Swali: Ni kwa nini wanachuoni hawakumkufurisha al-Ma´muun kwa kuzingatia ya kwamba hakuwa mjinga?

Jibu: al-Ma´muun alikuwa anatokamana na Banul-´Abbaas na kutoka katika familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Alikuwa anafanya taawili. Anaingia katika taawili. Walimdanganya. Mu´tazilah walimdanganya. Kwa ajili hiyo ndio maana akapewa udhuru. Allaah Atusamehe sisi na yeye.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (10) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/msrf–02041434.mp3
  • Imechapishwa: 27/06/2015