Swali: Niliswali leo pamoja na waislamu wengine swalah ya Maghrib na ´Ishaa kwa kuzikusanya katika wakati wa Maghrib kwa sababu ya mvua. Ni ipi hukumu ya hilo khaswa kwa kuzingatia kwamba njia hazina taabu kubwa, bali zimejengwa vizuri huku kukiwa na maji kidogo? Mwingine mfano wake anasema kuwa yeye ameswali katika msikiti wa al-´Ulyaa na wakakusanya kati ya Maghrib na ´Ishaa kisha akatoka. Je, amepata dhambi? Mwingine anauliza ni ipi hukumu ya kukusanya swalah katika hali ya kushuka mvua kubwa katika siku kama hii?
Jibu: Msingi wa kukusanya swalah mbili, Maghrib na ´Ishaa, kwa sababu ya mvua au utelezi ni jambo linalofaa. Hili walilifanya Salaf. Kwa hiyo halina neno. Zipo Hadiyth Swahiyh zinazojulisha kufaa kwa jambo hilo. Ikiwa eneo la msikiti lina mvua inayowaudhi watu wanapotoka au wanaporudi, kuna utelezi au matope yanayowasumbua, basi inafaa kukusanya. Ama ikiwa maeneo ya karibu na msikiti hayana madhara – hakuna mvua inayowadhuru watu, wala hakuna utelezi au tope – basi hakuna sababu ya kukusanya kwa sababu tu ya kuwepo athari ndogo ya mvua. Lakini ikiwa mvua inanyesha wakati wa swalah au kuna utelezi na tope unaowasumbua watu, basi ni sawa kukusanya.
Mwanafunzi: Vipi kuhusu swalah waliyoswali?
Ibn Baaz: Kulingana na vila mlivyosikia. Ikiwa walikuwa na udhuru, basi swalah yao ni sahihi. Ikiwa hawakuwa na udhuru, basi wanapaswa kuirudia.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3526/حكم-الجمع-بين-الصلاتين-بسبب-المطر
- Imechapishwa: 05/09/2026
Swali: Niliswali leo pamoja na waislamu wengine swalah ya Maghrib na ´Ishaa kwa kuzikusanya katika wakati wa Maghrib kwa sababu ya mvua. Ni ipi hukumu ya hilo khaswa kwa kuzingatia kwamba njia hazina taabu kubwa, bali zimejengwa vizuri huku kukiwa na maji kidogo? Mwingine mfano wake anasema kuwa yeye ameswali katika msikiti wa al-´Ulyaa na wakakusanya kati ya Maghrib na ´Ishaa kisha akatoka. Je, amepata dhambi? Mwingine anauliza ni ipi hukumu ya kukusanya swalah katika hali ya kushuka mvua kubwa katika siku kama hii?
Jibu: Msingi wa kukusanya swalah mbili, Maghrib na ´Ishaa, kwa sababu ya mvua au utelezi ni jambo linalofaa. Hili walilifanya Salaf. Kwa hiyo halina neno. Zipo Hadiyth Swahiyh zinazojulisha kufaa kwa jambo hilo. Ikiwa eneo la msikiti lina mvua inayowaudhi watu wanapotoka au wanaporudi, kuna utelezi au matope yanayowasumbua, basi inafaa kukusanya. Ama ikiwa maeneo ya karibu na msikiti hayana madhara – hakuna mvua inayowadhuru watu, wala hakuna utelezi au tope – basi hakuna sababu ya kukusanya kwa sababu tu ya kuwepo athari ndogo ya mvua. Lakini ikiwa mvua inanyesha wakati wa swalah au kuna utelezi na tope unaowasumbua watu, basi ni sawa kukusanya.
Mwanafunzi: Vipi kuhusu swalah waliyoswali?
Ibn Baaz: Kulingana na vila mlivyosikia. Ikiwa walikuwa na udhuru, basi swalah yao ni sahihi. Ikiwa hawakuwa na udhuru, basi wanapaswa kuirudia.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3526/حكم-الجمع-بين-الصلاتين-بسبب-المطر
Imechapishwa: 05/09/2026
https://firqatunnajia.com/salaf-na-kukusanya-swalah-kwa-sababu-ya-mvua-nyingi/