Swali: Ni ipi dalili yenu ya kuruhusu mgonjwa kuchanganya swalah ya Dhuhr na ´Aswr, na Maghrib na ´Ishaa?
Jibu: Kumepokelewa juu yake Hadiyth nyingi. Miongoni mwa dalili hizo ni Hadiyth ya Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alichanganya swalah akiwa Madiynah bila ya khofu wala mvua. Imekuja katika riwaya nyingine inayosema bila ya khofu wala safari. Hii inafahamisha kwamba sababu za kuchanganya swalah si khofu, mvua au safari tu, bali pia kuna sababu nyingine kama ugonjwa; na ugonjwa wenye mashaka una zaidi ya kupewa ruhusa.
Pia kuna Hadiyth ya Hamnah bint Jahsh (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimruhusu kuchanganya swalah kwa sababu ya kutokwa na damu ya maradhi na akamwambia kuwa hiyo ni katika chaguo bora kwake. Wanazuoni wakasema:
”Ikiwa kutokwa na damu ya ugonjwa, ambayo ni aina ya maradhi yenye tabu, imeruhusiwa kuchanganya swalah, basi maradhi mengine yanayosababisha uzito mkubwa kama homa kali na mfano wake pia yanaruhusu kuchanganya swalah.”
Kwa hiyo hapana vibaya akikusanya katika hali hiyo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3523ادلة-جمع-المريض-للصلاة
- Imechapishwa: 05/09/2026
Swali: Ni ipi dalili yenu ya kuruhusu mgonjwa kuchanganya swalah ya Dhuhr na ´Aswr, na Maghrib na ´Ishaa?
Jibu: Kumepokelewa juu yake Hadiyth nyingi. Miongoni mwa dalili hizo ni Hadiyth ya Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alichanganya swalah akiwa Madiynah bila ya khofu wala mvua. Imekuja katika riwaya nyingine inayosema bila ya khofu wala safari. Hii inafahamisha kwamba sababu za kuchanganya swalah si khofu, mvua au safari tu, bali pia kuna sababu nyingine kama ugonjwa; na ugonjwa wenye mashaka una zaidi ya kupewa ruhusa.
Pia kuna Hadiyth ya Hamnah bint Jahsh (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimruhusu kuchanganya swalah kwa sababu ya kutokwa na damu ya maradhi na akamwambia kuwa hiyo ni katika chaguo bora kwake. Wanazuoni wakasema:
”Ikiwa kutokwa na damu ya ugonjwa, ambayo ni aina ya maradhi yenye tabu, imeruhusiwa kuchanganya swalah, basi maradhi mengine yanayosababisha uzito mkubwa kama homa kali na mfano wake pia yanaruhusu kuchanganya swalah.”
Kwa hiyo hapana vibaya akikusanya katika hali hiyo.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3523ادلة-جمع-المريض-للصلاة
Imechapishwa: 05/09/2026
https://firqatunnajia.com/ni-ipi-dalili-ya-kumruhusu-mgonjwa-kukusanya-swalah/