Swali: Mfungaji akisafiri na akakusudia kurejea siku hiyohiyo – je, anapata ruhusa kama msafiri?
Jibu: Ana ruhusa mpaka pale atakaporejea. Atakaporejea basi atajizuilia. Lakini muda wa kuwa bado yuko safarini inafaa kwake kula na kuswali kwa kufupisha.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/audios/794/فتاوى-رمضانية
- Imechapishwa: 16/04/2023