03. Baadhi ya hukumu kuhusu swawm ya siku sita za Shawwaal

Ambaye anaidaiwa swawm basi anatakiwa kuanza kuifunga kisha akimaliza ndio afunge siku hizi. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule atakayefunga Ramadhaan kisha akaifuatishia [siku] sita za Shawwaal, basi anakuwa kama amefunga mwaka mzima.”[1]

Ambaye anadaiwa siku kadhaa za Ramadhaan haihakikishwi kwake ya kwamba amefunga Ramadhaan mpaka alipe siku hizo kisha baadaye ndio afunge siku sita hizo. Isitoshe ni kwamba mja ambaye ´ibaadah ni yenye kumuwajibikia anatakiwa kuharakisha kutekeleza wajibu na kuitakasa dhimma yake[2].

Udhahiri kutokana na maneno ya wanazuoni ni kuwa mwezi wa Shawwaal ukimalizika kabla ya mtu kufunga siku sita hizi basi hazitolipwa tena. Ni mamoja ameziacha kutokana na udhuru au ni pasi na udhuru. Kwa sababu ni Sunnah iliyopita wakati wake. Mwekaji Shari´ah ameiwekea muda maalum katika Shawwaal na hivyo basi fadhilah zake hazipatikani kwa mwenye kuzifunga katika kipindi kingine kwa kupita manufaa ya kuharakisha kuyafanya yale yanayopendeza kwa Allaah (Ta´ala). Ingelikuwa Shawwaal inalingana na miezi mingine basi kusingelikuwa na faida yoyote kuitaja. Allaah ndiye mjuzi zaidi.

[1] Muslim (164). Wanazuoni wamezungumzia juu ya Hadiyth hii kuishilia kwa Swahabah, jambo ambalo Imaam Ahmad pia amemili kwako. Yametajwa hayo na Ibn Rajab katika al-Latwaaif”, uk. 256 na pia tazama “Risaalah” ya al-´Alaaiy” juu ya Hadiyth hii.

[2] Tazama ”Fath-ul-Baariy” (03/280) ya Ibn Rajab. Amenakili maoni mawili kuhusu anayefunga kabla ya kulipa deni lake ambapo akasema:

”Lakini wanazuoni wengi wanaona kuwa inafaa.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtaswar Ahaadiyth-is-Swiyaam, uk. 85-86
  • Imechapishwa: 09/03/2023