Ni bora kujifunika wakati wa kuoga uchi?

Swali: Ni bora kujifunika wakati wa kuoga uchi?

Jibu: Hapana neno kuoga uchi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akioga uchi, Muusa alioga uchi na Ayyuub alioga uchi.

Swali: Mwenye kusema kuwa kuoga uchi inafaa lakini hata hivyo kujifunika ndio bora zaidi?

Jibu: Hapana. Hapana neno kuoga uchi. Kujifunika kunaweza kumtia uzito. Kwa sababu kujifunika kunaweza kuilowa nguo yake kwa maji.

Swali: Kwa hivyo hakuna vibaya?

Jibu: Jambo ni lenye usahali akiwa ndani ya chumba na hakuna yeyote anayemuona.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22301/هل-يشرع-التستر-حال-الاغتسال
  • Imechapishwa: 09/03/2023