Kuichelewesha Witr mpaka wakati wa Tahajjud

Swali: Wako baadhi ya watu wakati imamu anapomaliza kuswali Witr husimama na kuswali Rak´ah nyingine kwa hoja kuwa wanaichelewesha Witr yao mwishoni mwa usiku. Tunaomba utupe fatwa juu ya kitendo hichi.

Jibu: Hapana vibaya – Allaah akitaka. Anaweza kuiswali na akaswali mwishoni mwa usiku kile atachojaaliwa na itamtosha ile Witr ya kwanza. Akiswali na imamu mwanzoni mwa usiku na akaleta Rak´ah nyingine moja au kuifanya Witr yake mwisho wa usiku ni sawa – Allaah akitaka. Akiswali na wengine na kutoa salamu na wengine basi itamtosha Witr hiyo. Ikiwa atasimama tena mwishoni mwa usiku kile kiasi atachojaaliwa; Rak´ah mbili, nne, sita au nane ambapo ataleta Tasliym kila baada ya Rak´ah mbili na hatohitaji Witr nyingine kwa sababu inamtosha ile Witr ya kwanza aliyoswali.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/audios/794/فتاوى-رمضانية
  • Imechapishwa: 16/04/2023