Swali: Nimesoma katika gazeti la “Majallat-ud-Da´wah” ukisema kuwa inafaa kwa imamu na waswaliji kwa mfano kumuomba Allaah kinga dhidi ya Moto na kumuomba Allaah wakati kunaposomwa Aayah inayozungumzi rehema, jambo ambalo linafanywa na waswaliji wengi. Lakini nimekusikia tena ukisema katika “al-Jaamiy´ al-Kabiyr” ya kwamba haijuzu kwa yeyote kutamka ndani ya swalah na badala yake anatakiwa kusikiliza na kwamba kutamka inafaa katika swalah ya usiku peke yake. Naomba ufafanuzi.

Jibu: Haya yanafanywa katika swalah ya usiku. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika swalah ya usiku katika Aayah inayozungumzia rehema alikuwa akisimama na kumuomba Allaah amrehemu, Aayah inayozungumzia matishio ya adhabu anaomba amkinge na Aayah inayomtukuza Allaah anamtukuza. Hakuna ubaya bali ni Sunnah ikiwa anaswali usiku na akasimama maeneo hayo kama ambavo alikuwa akifanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni sawa na haya yanafanywa katika Tahajjud usiku, kisimamo cha usiku au katika Tarawiyh.

Kuhusu swalah ya Fajr hapana. Haikuhifadhiwa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alikuwa akisimama. Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisoma na hasimami. Lakini akiswali Tahajjud usiku na akasimama kwenye Aayah ya rehema, akaomba ulinzi katika Aayah ya matishio, akamtukuza Allaah katika Aayah ya matukuzo ni sawa. Bali ndio jambo linalopendeza lililofanywa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lilifanywa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika swalah ya usiku. Hudhayfah, Ibn Mas´uud na kikosi cha Maswahabah wengine (Radhiya Allaahu ´anhum) wamepokea hayo kutoka kwake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/audios/794/فتاوى-رمضانية
  • Imechapishwa: 16/04/2023