Ni lazima kulala na nia kwa ajili ya kufunga siku sita za Shawwaal?

Swali: Ni lazima kwa mtu kulala na nia kwa ajili ya kufunga zile siku sita za Shawwaal?

Jibu: Inajuzu kwake kufunga hata kama hakulala na nia. Kwani hii ni swawm ya sunnah. Inafaa kuweka nia mchana. Kwa sharti ya kwamba mtu asiwe alikula au kunywa baada ya kuingia alfajiri. Kulala na nia inahusiana na swawm ya faradhi peke yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (12) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdah%20Fiqh-19-10-1434_0.mp3
  • Imechapishwa: 30/09/2017

Turn on/off menu