Sababu ya Allaah kutanguliza mali kabla ya nafsi

Swali: Hadiyth ya Anas inayosema:

“Wapigeni jihaad washirikina kwa mali na ndimi zenu.”

Mpangilio huu ni kwa njia ya ubora?

Jibu: Ni lazima kufanya yote. Yote hayo ni lazima; kwa mali, nafsi na kwa ulimi.

Swali: Ni kwa nini kumetangulizwa mali?

Jibu: Mara nyingi Allaah ametanguliza mali katika Aayah nyingi. Manufaa yake ni yenye kuenea. Watu wananunua silaha kwa mali, wakatayarisha jeshi na wakawahudumia wapambanaji jihaad na mengine mengi. Mali ina manufaa mengi. Ndio maana Allaah katika maeneo mengi akaanza kuitaja mali mbele ya nafsi, isipokuwa katika Aayah ya “at-Tawbah”:

إِنَّ اللَّـهَ اشْتَرَىٰ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُم بِأَنَّ لَهُمُ الْجَنَّةَ ۚ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ

”Hakika Allaah amenunua kwa waumini nafsi zao na mali zao kwamba watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Allaah; wanaua na wanauawa.”[1]

Hapa ndipo ametanguliza nafsi mbele ya mali.

Ninachotaka kusema ni kwamba kupambana jihaad kwa mali kumeenea zaidi na kuna manufaa zaidi. Wakati mwingine kunahitajika mali na hakuhitajiki watu.

[1] 09:111

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23000/ما-الحكمة-من-تقديم-الجهاد-بالمال-في-الترتيب
  • Imechapishwa: 04/10/2023