Malaika kwenye nyumba zenye magazeti yenye picha

Swali: Je, Malaika hawaingii ndani ya nyumba ambayo kuna magazeti yenye picha?

Jibu: Kunakhofiwa hivo. Salama zaidi kwa muumini akate vichwa vya picha hizo. Azifute kwa kitu. Vichwa avipake rangi mpaka viondoke au avikate.

Swali: Afanye hivo kwa kila picha ilioko kwenye gazeti?

Jibiu: Vichwa vyake. Hivo ndio salama zaidi. Vinginevyo rahisi ni yeye kuyafukia. Ni sawa pia akikata vichwa vyake kwa kuviondosha au avipake rangi kama vile wino au rangi nyingine itakayoviondosha.

Swali: Vipi ikiwa anayasoma na akimaliza anayatupa?

Jibu: Ikiwa hayana faida ayapasue au ayazike.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22989/هل-صور-الصحف-مما-يمنع-دخول-الملاىكة
  • Imechapishwa: 04/10/2023