Swali: ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia akisema:

“Mimi na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tulikuwa tukioga kwenye chombo kimoja kilichokuwa kati yangu mimi na yeye kiasi cha kwamba mikono yetu ilikuwa ikipishana ndani yacho. Akishindana nami mpaka nafikia kusema: “Nibakishie [maji], nibakishi.” Tulikuwa katika hali ya janaba.”[1]

Je, hili linajulisha kuwa inafaa kwa wanandoa kuoga pamoja ingawa ni katika kutia wudhuu´ wa mchana? Kwa sababu wako wanazuoni wanaosema hili lilikuwa katika josho la usiku?

Jibu: Hapana, hili halina neno. Allaah amemhalalishia tendo la ndoa. Tendo la ndoa ni kubwa zaidi kuliko kutazama. Inafaa kwake mwanaume kumtazama mke na mwanamke kumtazama mume na wakaoga pamoja wakiwa uchi. Kwa sababu Allaah amemhalalishia mwanaume uchi wake mke na akamhalalishia mwanamke uchi wake mume. Hapana makosa ni mamoja usiku na mchana. Lakini wawe wamejificha mbali na watu.

[1] Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim, Abu ´Awaanah katika “as-Swahiyh” zao na muundo ni wa Muslim na nyongeza ni ya kwake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23419/حكم-غسل-الرجل-مع-زوجته-جميعا
  • Imechapishwa: 14/01/2024