Swali: Mwenye kumlaani mtu maalum kwa kufanya ghadhabu kwa ajili ya Allaah?

Jibu: Hapana, asimlaani muumini. Lakini amlingania katika kheri. Amlinganie, amnasihi na kumwelekeza katika kheri. Hata hivyo hapana neno kuwalaani makafiri kwa njia ya ujumla. Allaah amewalaani mayahudi, manaswara, watenda madhambi, madhalimu na wezi. Hili ni kwa njia ya kuenea au si mtu kwa dhati yake. Hapana vibaya kufanya hivo.

Hata hivyo anaweza kulaaniwa mtu kwa dhati yake haja ikipelekea kufanya hivo. Kwa mfano mtu huyo ni katika viongozi wa makafiri au mwenye kuwadhulumu watu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwalaani kundi la Quraysh kabla na baada ya suluhu ya Hudaybiyah wakati ilipozidi shari yao. Mfano wa Abu Lahab, ´Utbah bin Rabiy´ah na Abu Jahl bin Hishaam kutokana na ubaya wa ukafiri wao na dhuluma yao kwa watu. Vinginevyo mara nyingi na Sunnah inajulisha kutolaani kwa kadri inavyowezekana. Alipoambiwa: “Ee Mtume wa Allaah! Hakika Daws wamefika. Waombee kwa Allaah dhidi yao.” Akasema:

“Ee Allaah! Waongoze Daws na walete.”

Vilevile wakati (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoletewa bwana mmoja juu ya punda ambaye amekunywa pombe, mtu mmoja akamwambia: “Allaah amlaani! Ni mara ngapi ameletwa kwake.” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Usimlaani. Kwani hakika anampenda Allaah na Mtume Wake.”

Mtu anaweza kuwa ni mtenda dhambi lakini anayo mapenzi kwa Allaah. Kwa hivyo anatakiwa kuombewa uongofu na kusamehewa. Shaytwaan anashinda na matamanio humshinda mtu. Hapana uwezo wa kutikisika wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah. Awashauri familia yake, majirani zake na marafiki zake yaliyo na kheri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23417/حكم-من-لعن-شخصا-معينا-غضبا-لله
  • Imechapishwa: 14/01/2024