Rangi ya umanjano baada ya kutoka katika hedhi inaathiri swawm?

Swali: Shangazi yangu alisafika katika Ramadhaan kabla ya alfajiri kuingia ambapo akafunga siku hiyo. Aliposimama kuswali dhuhr akaona rangi ya umanjano/zambarau. Je, swawm yake ni sahihi?

Jibu: Ikiwa kusafika kulitokea kabla ya alfajiri kuingia halafu akafunga, basi swawm yake ni sahihi. Umanjano hauathiri kitu baada ya kusafika. ´Umm ´Atwiyyah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Tulikuwa hatuzingatii maji ya uchafu-uchafu na umanjano kuwa ni kitu baada ya kusafika.”[1]

[1] Abu Daawuud (307).

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/158)
  • Imechapishwa: 04/06/2017