Swawm ya aliyefunga baada ya kutoka katika uzazi kwa siku saba

Swali: Mke wangu amezaa mtoto  siku saba kabla ya Ramadhaan kuingia. Lakini hata hivyo akatwaharika kabla ya Ramadhaan kuingia. Je, swawm yake ni timilifu au ni lazima kulipa kwa kuzinga ya kwamba anasema kuwa alifunga akiwa ni msafi?

Jibu: Mambo yakiwa kama ulivosema ya kwamba mke wako alifunga Ramadhaan akiwa msafi basi swawm yake ni sahihi na wala haimlazimu kulipa.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/155-156)
  • Imechapishwa: 04/06/2017