Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Qur-aan ni hoja yako au dhidi yako.”

Kwa sababu Qur-aan ndio Kamba ya Allaah. Qur-aan ni hoja ya Allaah juu ya viumbe Vyake. Qur-aan ni hoja yako pale ambapo utaomba kupitia yenyewe kwa ajili ya kumfikia Allaah, utasimama na ya wajibu yake kwa kusadikisha maelezo yake, kutekeleza maamrisho yake na kujiepusha na makatazo yake, kuiadhimisha na kuiheshimu. Katika hali hii Qur-aan itakuwa ni hoja yako.

Lakini ikiwa mambo ni kinyume chake; uliisaliti Qur-aan na kuihama kimataamshi, kimaana na kimatendo na hukusimama na ya wajibu yake, basi itashuhudia dhidi yako siku ya Qiyaamah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/192)
  • Imechapishwa: 16/02/2023