Swalah ni nuru. Ni nuru kwa mja kwenye moyo wake, usoni mwake na ndani ya kaburi lake. Ndio maana utaona wengi miongoni mwa watu ambao wana nuru ni wale wenye kuswali sana na wenye kumcha zaidi Allaah (´Azza wa Jall).

Vilevile mtu anakuwa na nuru ndani ya moyo wake kwa kufunguliwa mlango wa maarifa ya kumtambua Allaah (´Azza wa Jall), hukumu za Allaah, matendo Yake, majina na sifa Zake. Vivyo hivyo nuru kwenye kaburi la mwanadamu. Kwa sababu swalah ndio nguzo ya Uislamu. Nguzo ikisimama imara jengo pia husimama. Vinginevyo jengo halisimami.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/190)
  • Imechapishwa: 16/02/2023