Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

… na Allaah akafaradhisha kwa viumbe wote – majini na watu – kumtii. Dalili ni Kauli Yake (Ta´ala):

قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُمْ جَمِيعًا

“Sema: “Hakika mimi ni Mtume wa Allaah kwenu nyinyi nyote.””[1]

Allaah kupitia kwake ameikamilisha dini. Dalili ni Kauli Yake (Ta´ala):

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا

”Leo nimekukamilishieni dini yenu na nimekutimizieni neema Yangu na nimekuridhieni kwenu Uislamu uwe ndio dini yenu.”[2]

Dalili ya kufa kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Kauli Yake (Ta´ala):

إِنَّكَ مَيِّتٌ وَإِنَّهُم مَّيِّتُونَ ثُمَّ إِنَّكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عِندَ رَبِّكُمْ تَخْتَصِمُونَ

“Hakika wewe utakufa na wao pia ni watakufa. Kisha hakika nyinyi siku ya Qiyaamah mbele ya Mola wenumtagombana.”[3]

MAELEZO

Kumtii Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni lazima kwa majini na watu wote. Yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Mtume wa Allaah kwenda kwa waarabu na wasiokuwa waarabu katika majini na watu. Majini wamefaradhishiwa mambo ya Shari´ah kama walivyofaradhishiwa watu. Dalili ni maneno Yake (Ta´ala):

وَإِذْ صَرَفْنَا إِلَيْكَ نَفَرًا مِّنَ الْجِنِّ يَسْتَمِعُونَ الْقُرْآنَ فَلَمَّا حَضَرُوهُ قَالُوا أَنصِتُوا ۖ فَلَمَّا قُضِيَ وَلَّوْا إِلَىٰ قَوْمِهِم مُّنذِرِينٍَ

”Wakati Tulipowaelekeza kwako kundi miongoni mwa majini wakisikiliza Qur-aan, walipoihudhuria walisema: “Nyamazeni [msikilize]!” Ilipokwisha [kusomwa], waligeuka kurudi kwa watu wao wakiwaonya.”[4]

وَأُوحِيَ إِلَيَّ هَـٰذَا الْقُرْآنُ لِأُنذِرَكُم بِهِ وَمَن بَلَغَ

“Nimefunuliwa Wahy hii Qur-aan ili nikuonyeni kwayo na kila itakayomfikia.”[5]

تَبَارَكَ الَّذِي نَزَّلَ الْفُرْقَانَ عَلَى عَبْدِهِ لِيَكُونَ لِلْعَالَمِينَ نَذِيرًا

“Amebarikika Yule ambaye ameteremsha Pambanuzi kwa mja Wake ili awe ni muonyaji kwa walimwengu.”[6]

Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) amesema:

“Dalili ya kufa kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)… “

Ameshakufa. Hata hivyo yuko hai uhai wa maisha ya ndani ya kaburi. Kiwiliwili chake kitukufu hakiliwi na ardhi. Bado ni kibichi na ni chenye kubaki. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika Allaah (´Azza wa Jall) ameiharamishia ardhi kula miili ya Manabii.”[7]

Ama watu wengine miili yao haibaki na hakuna kinachobaki isipokuwa عجب الذنب ambacho ni kifupa kilicho kwenye uti wa mgongo wa mtu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kila mwana wa Aadam huliwa na udongo. Isipokuwa عجب الذنب; ameumbwa kwacho na hutengenezwa kwacho.”[8]

Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) ametaja dalili ya kufa kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

إِنَّكَ مَيِّتٌ وَإِنَّهُم مَّيِّتُونَ

“Hakika wewe utakufa na wao pia ni watakufa.”

Baadhi ya watu huvutana ya kwamba hakufa. Vilevile dalili nyingine inayofahamisha juu ya kufa kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni maneno Yake (Ta´ala):

وَمَا مُحَمَّدٌ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ الرُّسُلُ ۚ أَفَإِن مَّاتَ أَوْ قُتِلَ انقَلَبْتُمْ عَلَىٰ أَعْقَابِكُمْ ۚ

“Muhammad si chochote isipokuwa ni Mtume tu [na] wamekwishapita kabla yake Mitume [wengine]. Je, akifa au akiuawa mtageuka nyuma ya visigino vyenu?”[9]

[1] 07:158

[2] 05:03

[3] 39:30-31

[4] 46:29

[5] 06:19

[6] 25:01

[7] Abu Daawuud (1047), an-Nasaa´iy (1374) na Ibn Maajah (1085). al-Haakim amesema:

”Hadiyth hii ni Swahiyh juu ya sharti za al-Bukhaariy” lakini hakuipokea.

[8] Muslim (2955).

[9] 03:144

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 103-104
  • Imechapishwa: 16/02/2023