Qur-aan ina maana ya dhahiri na iliyojificha?

Swali: Je, Qur-aan ina [maana ya] uinje na ya undani? Ni ipi hukumu ya yule mwenye kuamini hilo?

Jibu: Haya ni maneno ya Baatwiniyyah. Wao ndio wanasema kuwa Qur-aan ina [maana yake ya] undani wenye kutofautiana na uinje wake. Uinje wa Qur-aan hautofautiani na undani wake. Kamwe! Qur-aan ni naneno ya Mola wa walimwengu. Uinje wake hautofautiani na undani wake na kinyume chake.

Baatwiniyyah ndio ambao wanasema maneno haya. Wanasema kuwa uinje wa Qur-aan hautumiwi kama dalili. Dalili inatumiwa kwa undani wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (54) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-11-03.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020