Baadhi ya tafsiyr za Qur-aan zenye kuaminika

Swali: Mimi ninaogopa kuzungumza juu ya Allaah pasi na elimu au kusema juu ya maana ya Qur-aan na matokeo yake nikaja kutumbukia katika jambo hili ambalo nilahusiana na kuzungumza juu ya Allaah pasi na elimu. Je, inatosheleza kwangu kujifunza tafsiyr kupitia darsa zako na baadae nikawafikishia wengine?

Jibu: Qur-aan – himdi zote ni za Allaah – imefasiriwa kwa tafsiyr zenye kuaminika. Wasomee tafsiyr zake. Kuna tafsiyr ya Ibn Jariyr, tafsiyr ya Ibn Kathiyr na tafsiyr ya al-Baghawiy. Wasomee tafsiyr zenye kuaminika. Usifasiri wewe kwa mujibu wako ilihali huna elimu juu ya tafsiyr ya Qur-aan.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (54) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-11-03.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020