Jipime maarifa yako kuhusu swawm ya Shawwaal

Chemsha Bongo ya swawm ya Shawwaal

15:00

Ni lazima kwa mke kupata ruhusa kwa ajili ya kufunga siku sita za Shawwaal?

  • Ndio, kama unajua mume anaweza kukuhitaji mtake idhini kwanza
  • Hapana, ´ibaadah za Allaah zote zinatangulizwa mbele ya mume

Je, ni lazima kuanza kufunga siku sita za Shawwaal tarehe 2 Shawwal?

  • Ndio tarehe ambayo mtu analazimika kuanza kuifunga
  • Hapana ulazima, anaweza kuanza wakati wowote ndani ya Shawwaal

Nini malipo kwa ambaye atafunga Ramadhaan kikamilifu na akafuatishia swawm ya Shawwaal?

  • Ni kama amefunga mwaka mzima
  • Ataachwa huru na Moto

Ambaye amefanya tendo la ndoa kwenye swawm ya siku sita za Shawwaal au deni la Ramadhaan anapaswa kutoa kafara?

  • Atatoa kafara kama ni deni la swawm ya Ramadhaan
  • Hapana, kafara inakuwa ndani ya mwezi wa Ramadhaan pekee

Je, mume anapata dhambi akimjamii mkewe ndani ya swawm ya Shawwaal?

  • Ndio, anapata dhambi
  • Ni lazima kwa mume atoe kafara

Je, inafaa kufunga swawm ya Shawwaal siku ya ijumaa pekee?

  • Hapana, haifai kwa hali yoyote
  • Hapana, kwani ijumaa ni idi ya waislamu ya wiki

Je, mume anapata dhambi akimjamii mkewe katika swawm ya kulipa deni la Ramadhaan Shawwaal?

  • Hapana, hana dhambi ni haki yake
  • Anayo madhambi na lazima atoe kafara ya kuacha mtumwa huru

Je, inafaa kuanza kufunga siku sita za Shawwaal siku ya pili baada ya idi?

  • Anaweza tu kama alifunga siku zote za Ramadhaan
  • Ndio, inafaa na hapana vibaya

Je, ni lazima kufuatanisha wakati wa kufunga siku sita za Shawwaal?

  • Akifunga kwa kuachanisha hapata malipo yoyote
  • Ndio, inaruhusiwa

Bora katika kufunga siku ya Shawwaal kufuatanisha au kuachanisha?

  • Bora ni kufululiza
  • Bora ni kuachanisha

Je, ana malipo kusudiwa ya Shawwaal ambaye anafunga Shawwaal baada ya kumalizika mwezi kutokana na udhuru wa maradhi, hedhi n.k?

  • Kwa mujibu wa dalili, hapana
  • Itategemea nia yake

Je, swawm ya Ramadhaan ina mapungufu yoyote kama mtu hakufunga siku ya Shawwaal?

  • Ndio, ila tu kama ana udhuru wa kutofunga
  • Hapana, hakuna mahusiano

Je, mtu anaweza kufunga siku sita za Shawwaal baada ya kumalizika mwezi wa Shawwaal?

  • Anaweza kama tu alikuwa mgonjwa
  • Hapana

Je, inafaa kuanza kuweka nia ya siku sita za Shawwaal wakati wa mchana?

  • Ndio, inafaa kwa sharti asiwe amefanya kichenguzi chochote cha swawm baada ya alfajiri
  • Hakuna swawm ya kuweka nia katikati ya mchana

Je, inafaa kulipa siku ya Shawwaal ambayo mtu alifungua?

  • Hapana haifai
  • Swawm ya Sunnah hailipwi kabisa

Je, ana malipo mara 2 ambaye atakusudia kufunga siku sita za Shawwaal j.tatu, alkhamisi na swawm ya masiku meupe?

  • Kunatarajiwa iwe hivo, lakini haina uhakika
  • Haijuzu kabisa kufanya hivo

Anaanza kufunga swawm ipi ambaye anadaiwa swawm ya nadhiri au nyingine ya wajibu na anataka kufunga Shawwaal?

  • Ataanza na swawm ya Shawwaal
  • Ataanza na swawm ya nadhiri

    Je, inafaa kwangu kufungua swawm ya Shawwaal?

    • Ndio, inafaa kufungua swawm ya Sunnah
    • Akifungua anapata dhambi

    Mtu anaweza kufunga siku sita za Shawwaal mwishoni mwa mwezi wa Shawwaal?

    • Ndio, muhimu iwe ndani ya mwezi wa Shawwaal
    • Hana malipo anayefunga mwishoni mwa Shawwaal

    Je, ambaye hakukamilisha siku zote za Ramadhaan anapata malipo ya kufunga mwaka mzima?

    • Ndio, muhimu afunge siku sita
    • Hapana, ni lazima akamilishe deni lake la Ramadhaan kwanza
    • Atapata malipo nusu

    Je, inafaa kuunganisha swawm ya siku sita za Shawwaal baada ya kumaliza masiku yangu niliyokuwa nadaiwa Ramadhaan?

    • Ndio, inafaa
    • Hapana, haifai
    • Lazima apumzike siku kadhaa kabla ya kuanza siku sita za Shawwaal