Pale unapoanza kutembea peke yake

ar-Raajihiy: Katika Hadiyth inayosema:

“Akafanya kwenye Marwah kama ulivyofanya katika Swafaa.”

Je, maana yake ni kwamba anasema:

إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِن شَعَآئِرِ اللّهِ

“Hakika vilima vya Swafaa na Marwah ni katika alama za Allaah.”[1]

Jibu: Hapana, alifanya juu ya Marwah kama alivyofanya katika Swafaa katika du´aa, Dhikr na kunyanyua mikono yake. Vinginevyo mtu anasoma Aayah hiyo pale anapoanza peke yake.

[1] 02:158

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24997/هل-يشرع-على-المروة-مثل-ما-يفعل-في-الصفا
  • Imechapishwa: 24/01/2025